Haber Giriş:
Joe Biden aomba msaada kwa viongozi wa dini

Rais wa Marekani, Joe Biden, amewahimiza viongozi wa dini kuhamasisha jamii
Rais wa Marekani, Joe Biden, amewahimiza viongozi wa dini kuhamasisha jamii zao kupewa chanjo dhidi ya virusi vya corona.
Joe Biden alizungumza na viongozi wa dini zaidi ya elfu hapo jana.
Katika mkutano huo, Biden alisisitiza kwamba viongozi wa dini wana nafasi muhimu sana katika vita dhidi ya Covid-19.
"Ninawahimiza muwahamasishe watu wapate chanjo dhidi ya corona.", alisema Biden.
...-
16.04.2021
-
16.04.2021